IGP Wambura safarini India

0
188

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Camillus Wambura alipotembelea ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini India, na kufanya mazungumzo na balozi wa Tanzania nchini humo Anisa Mbega.

Katika mazungumzo yake na balozi Mbega wamejadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutafuta fursa nchini India hasa za kimasomo, ili kuwawezesha askari polisi wa Tanzania kufanya kazi kwa umahiri zaidi ikiwemo matumizi ya sayansi na teknolojia katika kuzuia uhalifu na wahalifu.

IGP Wambura na ujumbe wake upo New Delhi, India, kuhudhuria mkutano mkuu wa Shirikisho la Polisi la Kimataifa (INTERPOL).