D’jaro wa TBC arejea nchini na tuzo

0
407

Mtangazaji wa kipindi cha Papaso cha TBC FM, D’jaro Arungu maarufu Baba Mzazi, amewasili usiku huu katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam na kupokelewa na wasanii pamoja na wasikilizaji wa redio akitokea Lusaka Zambia ambako alienda katika tuzo za Zikomo.

D’jaro ameshinda tuzo ya Mtangazaji Bora wa Redio barani Afrika katika usiku wa Zikomo Oktoba 15, 2022.

Tuzo za kimataifa za Zikomo hutolewa kwa mtu ama taasisi zinazofanya vizuri zaidi kwenye maeneo yao kama uandishi wa habari, sanaa na ujasiriamali.