Benzema ashinda Tuzo ya Ballon d’Or 2022

0
625

Karim Benzema msimu uliopita alifanya vizuri akiwa na Real Madrid na timu ya Taifa ya Ufaransa hivyo kumfanya kuwaacha mbali washindani wake kwenye tuzo ya mwaka huu ya Ballon d’Or.

  1. Karim Benzema
  2. Sadio Mané
  3. Kevin De Bruyne
  4. Robert Lewandowski
  5. Mohamed Salah
  6. Kylian Mbappé

Mwaka uliopita Karim Benzema alimaliza katika nafasi ya nne kwenye tuzo za Ballon d’Or nyuma ya Lionel Messi, Robert Lewandowski na Jorginho.

Hii ni tuzo yake ya kwanza Benzema kushinda.

Sherehe za tuzo hizo zimefanyika usiku wa leo Oktoba 17, 2022 katika jiji la Paris katika Ukumbi wa Théâtre du Châtelet.

Hizi ni tuzo za 66 tangu zianze kutolewa mwaka 1956.

Ballondor #Ballondor2022 #TBCupdates #TBConline