Kigoma kuunganishwa kwa barabara za lami

0
251

Rais Samia Suluhu Hassan leo amezindua barabara ya Kidahwe – Kasulu yenye urefu wa kilomita 63 ambayo inajengwa kwa kiwango cha lami.

Pia Rais Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Kabingo – Kasulu – Manyovu yenye urefu wa kilomita 260.6.

Akizungumza na wakazi wa mkoa wa Kigoma ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku nne mkoani Kigoma, Rais Samia amesema kuzinduliwa kwa barabara hizo za lami pamoja na ufunguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo kunakwenda kuufanya mkoa huo kuwa wa mkakati kibiashara.

“Umeme unakuja, barabara zinakuja Kigoma inakwenda kuwa mkoa wa kimkakati.” amesema Rais Samia

Aidha, Rais Samia Suluhu Hassan amefungua chuo cha ualimu Kabanga na kuwataka wakazi wa mkoa wa Kigoma kutumia vizuri fursa zinazoendelea kutolewa katika sekta ya elimu mkoani humo.