Mkutano mkuu wa CPC waanza Beijing

0
1113

Mkutano mkuu wa 20 wa wajumbe wote wa chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ambacho ni chama tawala nchini humo umeanza mjini Beijing.

Mkutano huo unaofanyika kuanzia hii leo hadi tarehe 22 mwezi huu, unahudhuriwa na wajumbe zaidi ya elfu mbili.

Mkutano huo utasikiliza na kuchunguza ripoti ya Kamati Kuu ya 19 ya CPC na ripoti ya kamati ya ukaguzi wa nidhamu ya kamati kuu hiyo, kuchunguza na kupitisha marekebisho ya katiba ya chama, kuchagua na kuunda awamu mpya ya kamati kuu ya chama na kamati ya ukaguzi wa nidhamu ya kamati kuu hiyo.

Tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya watu wa China, chama cha Kikomunisti chenye historia ya miaka 101 kimeendelea kutawala nchi hiyo huku kikiwa na wanachama zaidi ya milioni 96.

Mkutano mkuu wa wajumbe wote na kamati kuu inayochaguliwa kwenye mkutano huo, ni mamlaka za juu zaidi za uongozi za CPC.

Mkutano mkuu wa wajumbe wote wa CPC unafanyika kila baada ya miaka mitano.