Watumiaji wa facebook watahadharishwa

0
1472

Kampuni ya Meta imewatahadharisha watumiaji wa Facebook ambao wanaweza kuwa wamehatarisha usalama wa akaunti zao bila kujua kwa kupakua na kuweka wazi taarifa zao binafsi kupitia programu hasidi.

Watafiti wa usalama kutoka kampuni ya Tech Giant walipata zaidi ya programu 400 za Android na iOS mwaka huu ambazo ziliundwa kuiba taarifa za kuingia kwenye akaunti ya Facebook na kuathiri akaunti za watumiaji hao.

Programu hizo ziliorodheshwa kwenye mtandao wa Google Play Store na Apple App Store na kufichwa kama vihariri picha, michezo, huduma za VPN, programu za biashara na huduma zingine ili kuwalaghai watu wazipakue na kuzitumia.

“Hii ni nafasi yenye adui na upinzani mkubwa kwanj wakati wataalamu wetu wanafanya kazi ya kugundua na kuondoa programu hizo, baadhi ya programu hizo huepuka kutambuliwa kwa kujiingiza kwenye duka la programu halali,” David Agranovich, mkurugenzi wa Usumbufu na Matishio wa Meta alisema katika chapisho la blog siku ya Ijumaa.

Aidha amesema zimefanyika jitihada za kuripoti programu hizo hasidi kwa kampuni ya Apple na Google na mafanikio yameonekana kwani zipo programu zilizoondolewa kutoka kwa maduka mtandao ya programu kabla ya ripoti yao kuchapishwa.

Kulingana na kampuni ya Meta, programu hasidi zinatumia mbinu ya kuuliza watumiaji kuingia Facebook kupitia programu hizo hivyo mtumiaji akishafanya hivyo, programu hasidi itaiba jina la mtumiaji na nenosiri lake.

Ameongeza kusema kuwa mara tu baada ya maelezo hayo kuwekwa na mtumiaji, maelezo hayo huibiwa hivyo wavamizi wanapata nafasi ya kuzifikia akaunti za watumiaji pamoja na maelezo yao ya faragha na orodha ya marafiki.

Hata hivyo kampuni ya Meta imependekeza kwamba iwapo watumiaji wanaodhani kuwa huenda wamepakua moja ya programu hasi ni vyema wakabadilisha nywila za akaunti zao ili kuwa salama zaidi
na baada ya hilo waziripoti programu hizo kwa kwa kampuni ya Meta