Serikali yakiri afya ya akili ni tatizo kubwa

0
229

Serikali imesema kuna umuhimu wa kuangalia namna ya kutoa huduma za kisaikolojia na afya ya akili, kutokana na matukio mbalimbali yanayotokea nchini.

Kauli hiyo ya serikali imetolewa mkoani Dar es Salaam na waziri wa Afya Ummy Mwalimu, wakati wa kongamano la kwanza la kitaifa la afya ya akili ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya afya ya akili hii leo.

Pia ameshauri kuangaliwa uwezekano wa kuwa na vituo vya ushauri wa kisaikolojia, ili kuwaepusha vijana wengi kutumbukia kwenye sonona.

Waziri Ummy Mwalimu amewataka washiriki kutumia kongamano hilo la kwanza la kitaifa la afya ya akili,
kutoa maoni ya nini kifanyike kukabiliana na changamoto ya afya ya akili ambayo imekuwa tatizo kubwa kwenye jamii.

Amesema kwa upande wa Serikali inalichukulia suala hilo la afya ya akili kwa uzito mkubwa, na ndio sababu suala hilo liimeweka kwenye mpango.

Waziri Ummy amesema kuanzia sasa mpango wa Taifa wa magonjwa yasiyoambukiza utafahamika kama mpango wa Taifa wa magonjwa yasiyoambukiza, afya ya akili na ajali.