Picha: Sherehe za Maulid Kitaifa

0
222

Sherehe za Maulid Kitaifa zimefanyika kitaifa katika viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo mgeni alikuwa Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar Bin Zubeir.

Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu waliojitokeza katika viwanja vya Mnazi Mmoja, kusherehekea mazazi ya Mtume Muhammad (SAW) yanayoadhimishwa leo ambapo kitaifa yanafanyika mkoani Dar es Salaam.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam Ramadhan Madabida (kulia), akiwa na Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania Sheikh Hemed Jalala katika viwanja vya Mnazi Mmoja kusherehekea mazazi ya Mtume Muhammad (SAW) yanayoadhimishwa kitaifa mkoani Dar es Salaam.


Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demkorasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar Salum Mwalimu (kulia) akiwa na Katibu wa Kamati ya Amani Askofu Dkt. Israel Maasa katika viwanja vya Mnazi Mmoja kusherehekea mazazi ya Mtume Muhammad (SAW) yanayoadhimishwa kitaifa mkoani Dar es Salaam.