Mchango wa sekta ya madini wazidi kuimarika nchini

0
329

Mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa umeendelea kuimarika kutokana na kuongezeka kwa usimamizi wa shughuli mbalimbali za madini ambapo mwaka 2021 ulifikia asilimia 7.3 na sasa ukuaji wake umefikia asilimia 9.6.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji katika kilele cha Maonesho ya 5 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini katika viwanja vya Bombambili mkoani Geita.

Dkt. Kijaji amesema Sekta ya Madini ni muhimu kwenye mchango wa uchumi wa Taifa ambapo ameitaka Wizara ya Madini kuendelea kuisimamia sekta hiyo kwa lengo la kuongeza mchango wake kwenye Pato la Taifa.

Aidha, Dkt Kijaji amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa nia yake ya dhati ya kuleta mabadiliko chanya kwenye Sekta ya Madini kwa kuvutia wawekezaji wengi zaidi kutoka ndani na nje ya nchi