Bodi yaahidi kusimamia maslahi ya TBC

0
125

Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Stephen Kagaigai ameahidi kusimamia maslahi mapana ya shirika hilo, ili liwe na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake.

Akizungumza mkoani Dar es Salaam mbele ya waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo mpya, Kagaigai pamoja na wajumbe wa bodi hiyo wameahidi kusimamia kikamilifu mipango na maendeleo ya TBC.

Kagaigai ameongeza kuwa bodi hiyo itaanza kazi haraka iwezekanavyo, na itakuwa na mipango ya muda mfupi, wa kati na muda mrefu ili kuwezesha ufanisi wa kazi na maendeleo ya shirika hilo.