Mkutano wa UNWTO wafana

0
163

Picha mbalimbali kutoka kwenye mkutano wa 65 wa Shirika la Utalii Duniani (UNWTO) Kamisheni ya Afrika unaoendelea jijini Arusha.

Mkutano huo uliofunguliwa rasmi hii leo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, unafanyika kwa muda wa siku tatu ukiwa unahudhuriwa na washiriki kutoka nchi 33 wakiwemo wadau wa utalii na Mawaziri wa utalii wa nchi hizo.

UNWTO ilianzishwa mwaka 1946 chini ya Umoja wa Mataifa, kwa lengo la kutangaza utalii unaowajibika, endelevu na unaofikiwa na watu wote na mpaka sasa ina wanachama 160.