UVIKO-19 ni somo kwa wote

0
269

Rais Samia Suluhu Hassan amesema janga la UVIKO – 19 limetoa somo kubwa kwa dunia, la namna ya kukabiliana na majanga mbalimbali.

Rais Samia ametoa kauli hiyo huko Doha, Qatar,
wakati wa ufunguzi wa mkutano wa dunia katika ubunifu wa masuala ya afya.

Amesema kwa upande wa Tanzania, janga hilo la UVIKO – 19 limeifanya serikali kuandaa mikakati itakayosaidia kuwaandaa wataalamu wa ndani ili wawe tayari muda wote
kukabiliana na majanga hayo tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Amesema jambo ambalo dunia inatakiwa kufahamu ni kwamba janga la UVIKO -19 halina athari kwa sekta ya afya pekee bali kwa sekta zote, hivyo unahitajika ushirikiano wa pamoja katika kukabiliana nalo.

Rais Samia pia amesisitiza umuhimu wa kupatiwa chanjo dhidi ya UVIKO – 19 kwa wananchi wote, pasipo kujali wapi walipo.

Amesema anatambua na kuthamini mchango unaotolewa kwa Tanzania na wadau mbalimbali wa sekta afya, na kwamba serikali itaendelea kushirikiana na wadau hao.