Yanga SC inaendeleza ubabe kwenye Ligi Kuu ya NBC baada ya kuichapa Ruvu Shooting FC magoli 2-1 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.
Magoli ya Yanga yamefungwa na Feisal Salum na Bakari Mwamnyeto huku goli la pekee la Ruvu Shooting likifungwa na Rolland Msonjo dakika za lala salama.
Kwa ushindi huo Yanga imepanda hadi nafasi ya pili ikiwa na alama 13, sawa na Simba SC lakini zikitofautiana na kwa magoli ya kufunga na kufungwa, huku Wazee wa Mpapaso ikiwa nafasi ya nne baada ya kujikusanyia alama 9.