Dkt. Rioba atahadharisha upotoshaji kwenye mitandao ya jamii

0
2604

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC) Dkt. Ayub Rioba amewataka waandaaji na watayarishaji wa vipindi vya elimu kwa umma kutumia vema mitandao ya kijamii bila upotoshaji wa habari.

Dkt. Rioba ametoa kauli hiyo jijini Arusha wakati wa mkutano wa 102 wa washitiri wa vipindi vya elimu kwa umma, ambapo amesema wao ni watu muhimu wanaoaminiwa na taifa hivyo ni vema wakawa makini katika kufikisha ujumbe kwani hivi sasa kuna wimbi kubwa la upotoshaji wa taarifa zinazotolewa kwa jamii kupitia mitandao.

Washitiri kutoka katika idara na taasisi mbali mbali za umma wanakutana jijini Arusha kwa siku Saba kwa lengo la kujielimisha kutoka kwa wataalamu waliobobea kuhusu uandaaji wa vipindi kwa mfumo wa kisasa, mabapo Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ni wadhamini wakuu wa mkutano huo ulioandaliwa na TBC.

Akiwasilisha mada Mkurugenzi mkuu wa TBC Dkt Rioba amesema teknolojia ya kidigiti imeleta mabadiliko hivyo ni vyema waandaaji wa vipindi wakaitumia vema.

Afisa Habari wa Wakala wa Barabara nchini Aisha Malima amewasilisha mada kuhusu utekelezaji wa ujenzi wa barabara kuelekea uchumi wa viwanda ambapo amesema wakala umejipanga vema katika kukarabati na kujenga barabara nchini.
Mkurugenzi wa Huduma za Redio –TBC-AISHA DACHI,amesema mkutano huo utatumika kuwajengea uweledi washitiri hao katika kuelekea uchumi wa viwanda.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here