Jukwaa la biashara na uwekezaji

0
893

Matukio mbalimbali katika picha yakionesha Jukwaa la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Italia lililofanyika Zanzibar, ambapo Mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Othman Masoud Othman.

Wakati wa jukwaa hilo lililoshirikisha wafanyabiashara kutoka Tanzania na wengine zaidi ya mia moja kutoka Italia, mikataba mitano ya ushirikiano kati ya kampuni za Zanzibar na Italia imetiwa saini.

Jukwaa hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Mudrik Ramadhan Soraga, Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mahmoud Thabit Kombo na Balozi wa Italia nchini Tanzania Marco Lombardi.

Hapo kesho jukwaa kama hilo linatarajiwa kuzinduliwa kwa upande wa Tanzania Bara, uzinduzi utakaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) kilichopo mkoani Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi atakuwa waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji.