Jecha DPP Zanzibar

0
195

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi, amemteua Mgeni Jailani Jecha kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar (DPP) katika ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora.

Kabla ya uteuzi huo Mgeni alikuwa Mkurugenzi Idara ya Mipango, Uendeshaji na Rasilimali Watu katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu.

Uteuzi huo umeanza leo Septemba 28, 2022.