Bodi ya Hifadhi ya Ngorongoro yazinduliwa

0
241

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Pindi Chana leo Septemba 28, 2022 amezindua rasmi Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) jijini Arusha.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo, Dkt. Chana amesema Serikali chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaimani kubwa na Bodi hiyo katika kuleta maendeleo ya Mamlaka ya Hifadhi Ngorogoro na sekta ya Utalii kwa ujumla.

Amesema anataraji kuona Bodi hiyo yenye wajumbe wenye elimu za juu na uzoefu mkubwa chini ya Mwenyekiti Jenerali Mstaafu Venance Mabeyo itabuni vyanzo vipya vya Utalii ili kwendana na kasi ya matokeo Chana ya kazi nzuri iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Filamu ya The Royal Tour.

Awali akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Ndugu Juma Mkomi ameithibitishia Bodi hiyo kuwa Wizara itaendelea kutoa ushirikiano ili malengo yaliyokusudiwa yaweze kufikiwa.