Mradi wa SANAAPRO wazinduliwa

0
1217

Balozi wa Ufaransa nchini Nabil Hajlaoui, leo amezindua mradi wa SANAAPRO wenye lengo la kusaidia tasnia ya ubunifu nchini.

Akizindua mradi huo ambao umetengewa shilingi bilioni 1.2 Balozi Nabil amesema, mradi huo ni kipaumbele cha ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania katika kusaidia tasnia ya ubunifu.

Katika uzinduzi huo uliofanyika mkoani Dar es Salaam, Tanzania itafaidika na mradi huo kwa kujumuisha watu kutoka makundi mbalimbali, ikiwemo wajasiriamali, wanawake na vijana, viongozi kutoka mashirika ya kiraia na mabingwa wa michezo.

Mradi huo wa SANAAPRO utakuwa na kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuratibu mafunzo kwa wasanii 72, kuzalisha filamu fupi mbili zenye ubora wa kimataifa, kuratibu mafunzo kwa mafundi 70 kwenye maeneo ya sauti, mwanga na usimamizi pamoja na kuandaa mijadala kuhusu sekta ya ubunifu.