Wasiojulikana wahujumu miundombinu ya umeme

0
140

Wilaya za Kakonko, Kibondo, Kasulu na Buhigwe mkoani Kigoma hazina huduma ya umeme, baada ya watu wasiojulikana kufanya hujuma katika miundombinu ya umeme kwenye kijiji cha Itumbiko wilayani Kakonko.

Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Kigoma Mhandisi Jafari Mpina amesema, watu hao wasiojulikana wamekata na kung’oa baadhi ya vipuri pamoja na kuchoma moto miundombinu ya umeme kwa makusudi.

Pia wameacha ujumbe unaosema kuwa, kama hawatapatiwa huduma ya umeme katika eneo la Itumbiko wataendelea kuchoma moto nguzo.