Kiboko auawa baada ya kuzua taharuki Morogoro

0
2224

Kiboko anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 na 25 ameuawa kwa kupigwa risasi  na askari wa mamlaka ya wanyamapori (TAWA) baada ya kuzua tafrani kwa wakazi wa kata ya Kihonda Manispaa ya Morogoro alipoonekana akirandaranda majira ya alfajiri.

Afisa kutoka TAWA, Privatus Kasisi amesema kiboko huyo anadaiwa kutokea Mto Wami na kupoteza uelekeo  hadi alipobukia mto mdogo uliopo kata ya Kihonda.

Kasisi amesema askari wa Mamlaka hayo wamelazimika kumdhibiti  kwa kumuua kwa risasi mnyama huyo ili asisababishe madhara kwa binadamu.

Kiboko huyo ambaye safari yake ya mwisho iliishia katika ofisi ya kata ya Kihonda ana kilo zaidi ya 2500, ambapo alikatwakatwa na kugawiwa kwa wananchi waliokuwa jirani kwa kitoweo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here