Windows 11 yatoa vipengele vipya kwa watumiaji wake

0
1487

Ni takribani mwaka mmoja sasa tokea kampuni ya Microsoft izindue toleo jipya la mfumo wa uendeshaji wa kompyuta ‘Windows 11.’

Siku za hivi karibuni kampuni hiyo ya teknolojia imezindua rasmi sasisho lake la kwanza kwa mfumo wa uendeshaji wa kompyuta ‘Operating System.’

Panos Panay, Afisa mkuu wa bidhaa wa Windows kwa kampuni ya Microsoft, ameeleza katika moja ya blogu kuwa sasisho hilo linapatikana bila malipo kwa watumiaji wa sasa wa Windows 11, kwa zaidi ya nchi 190.

Panay ameeleza kwa kina jinsi sasisho hilo linalenga kufanya kazi kwenye Kompyuta ili iwe rahisi na salama zaidi.

Akifafanua kipengele kipya katika sasisho hilo kinachoitwa “Smart App control” hutumia Akili Bandia (AI) kuzuia programu hatarishi au zisizoaminika kufanya kazi kwenye vifaa hivyo kuipelekea Windows 11 kuwa mfomo wa uendeshaji wa kompyuta salama zaidi.

Mabadiliko mengine ameeleza kuwa ni pamoja na uboreshaji wa programu ya mipangilio ya muonekano wa ‘screen’ ya kompyuta ambayo huwasaidia watu kuboresha mtazamo wao wanapohitaji kufungua vitu vingi kuoneka kwenye kioo cha kompyuta yake kwa wakati mmoja.

Vilevile mfumo huo umeboresha kwa kuweka kipengele cha utulivu ‘do not disturb’ ili kusaidia kupunguza usumbufu unaomuondoa mtumiaji wa kompyuta kwenye kazi zake.

Hata hivyo Pany ameeleza kipo kipengele kipya kinachoitwa ‘Windows Studio Effects’ ambacho kwa kutumia teknolojia bandia kimeboresha simu za video na simu za sauti pekee kusaidia kuchuja sauti kwa kuondoa kelele za mazingira pamoja na kuinua macho ya mzungumzaji ili kuyafanya yaonekane yanatazama moja kwa moja kwenye kamera wakati ‘video call’ zikifanyika.