Waziri wa zamani ahukumiwa kifo

0
224

Aliyekuwa Waziri wa Sheria wa China, Fu Zhenghua amehukumiwa adhabu ya kifo baada ya kupatikana na hatia ya kupokea rushwa ya Yuan milioni 117 (zaidi za shilingi bilioni 77 za Tanzania), akiwa mtumishi wa umma.

Habari kutoka nchini China zinaeleza kuwa, hukumu hiyo inaweza kutekelezwa ndani ya kipindi cha miaka miwili au kuwa kifungo cha maisha baada ya miaka miwili kumalizika.

Pamoja na hukumu hiyo, Zhenghua amefukuzwa uanachama katika chama tawala cha nchini China – CPC.

Pia ameondolewa haki ya kushiriki shughuli zote za kisiasa za nchini China maisha yake yote na mali zake zote zimetaifishwa.