Ally Mayay kukaimu Ukurugenzi wa Michezo

0
195

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa amemteua Ally Mayay Tembele kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo.

Mayay ambaye kwa sasa ni Afisa Mwandamizi katika Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, amehamishiwa wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na kuruhusiwa kukaimu majukumu hayo kwa mujibu wa kibali cha ofisi ya Rais Utumishi.

Ally Mayay anachukua nafasi ya Yusuph Singo aliyepangiwa majukumu mengine na kwamba uteuzi wake umeanza leo Septemba 20, 2022.