“Panya road” wawaibua wabunge

0
221

Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson ameiagiza Serikali kuchukua hatua za haraka kushughulikia tatizo la vikundi vya uhalifu maarufu kama Panya Road, vilivyoibuka hususani katika mkoa wa Dar es salaam.

Spika ametoa agizo hilo kwa Serikali, baada ya Mbunge wa Viti maalum Bahati Ndingo na Mbunge wa jimbo la Segerea, Bonna Kamoli kumuomba Spika aruhusu Bunge lijadili jambo la dharura linalohusu usalama wa raia na kuibuka kwa vikundi vya uhalifu.

Akijibu hoja hizo Spika Dkt. Tulia amesema jambo hilo lipo chini ya serikali na kwamba wanatakiwa kulishughulia kwa haraka ili lisiendelee kuathiri usalama wa raia.