Dkt. Mwinyi amwakilisha Rais Samia Angola

0
850

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo anamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika sherehe za kuapishwa Rais Mteule wa Angola, Joao Manuel Goncalves Lourenco pamoja na Makamu wake Esperanca Maria Eduardo Franscisco da Costa.

Sherehe hizo zinatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Bara la Afrika na nje ya bara hilo.

Tayari Dkt. Mwinyi amewasili jijini Luanda, Angola kushiriki katika sherehe hizo.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Angola Quatro de Fevereiro, Rais Mwinyi na ujumbe wake amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Tete Antonia.