Tanzania katika mkutano wa 51 wa haki za binadamu

0
690

Mkutano wa 51 wa Baraza la Haki za Binadamu unaifanyika katika Umoja wa Mataifa Geneva, Uswisi ambapo ujumbe wa Tanzania unaongozwa katibu mkuu wa wizara ya maliasili na Utalii Profesa Eliamani Sedoyeka na Balozi wa Tanzania Geneva Maimuna Tarishi.

Pamoja na kushiriki vikao hivyo lakini pia kutakuwa na vikao vya pemebezeni.

Miongoni mwa Ajenda ambazo Tanzania imejipanga kuzungumzia ni pamoja na Haki ya Maendeleo kwenye Elimu, Afya, makazi, maji salama na Usafi.

Itaongelea pia athari za Uviko 19 hasa katika sekta ya Utalii na mikakati madhubuti iliyowekwa ya kudhibiti uchumi dhidi ya janga la Kovid 19, ikiwemo kuhimiza utoaji wa chanjo ya uviko na kutangaza Nchi kupitia filamu ya Royal Tour.