Rais Samia atunukiwa Tuzo Nigeria

0
143


Rais Samia Suluhu Hassan amepokea tuzo ya heshima ya Pyne Africa Awards 2022 katika hafla iliyofanyika kwenye viunga vya Eko Hotels na Suites, jijini Lagos, Nigeria.

Rais Samia ametunukiwa tuzo hiyo baada ya kuchaguliwa kama Rais bora muwajibikaji katika kuiendeleza sekta ya utalii barani Africa.

Tuzo hii imepokelewa na Balozi wa Tanzania chini Nigeria, Dk. Benson Bana kwa niaba ya Rais. Halfa hii ilihudhuriwa pia na Meya Mkuu wa Zanzibar, Mahomoud Mussa na Mwenyekiti wa Tume ya Utalii Zanzibar, Rahim Bhaloo.

Aidha Rais, wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi amepokea tuzo ya heshima kwa kutambua mchango wake wa mfano katika kukuza sekta ya Utalii Zanzibar ambayo ni kivutio cha Utalii.