Dabi ya Mbeya Hakuna mbabe

0
230

Mechi kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Mbeya City imemalizika kwa sare ya kufungana goli moja kwa moja katika dimba la Sokoine jijini Mbeya.

Mbeya City walitangulia kupata goli dakika ya 7 kupitia kwa Hassan Maulid na dakika za lala salama Prisons wakakomboa kupitia kwa Khamis Mcha.

Kwa matokeo hayo Mbeya City wanasogea nafasi ya nne huku Tanzania Prisons wakiwa nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.