Wajumbe wa bodi ya TBC wateuliwa

0
176

Kufuatia uteuzi wa Stephen Kagaigai kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amefanya uteuzi wa wajumbe wa bodi hiyo.

Waziri Nape amewateua Mwanjaa Lyezia, Justina Mashiba, Innocent Mungi na Amina Mollel kuwa Wajumbe wa bodi hiyo ya TBC.

Wengine ni Dkt. Hidelbrand Shayo, Tuma Abdallah na Cosmas Mwaisombe.