Halmashauri ya wilaya ya Mbeya imekabidhi mikopo yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 240 kwa vikundi Kumi na Vitano vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu vilivyopo katika halmashauri hiyo.
Hafla ya kukabidhi mikopo hiyo imefanyika katika mji mdogo wa Mbalizi ambapo Mkuu wa wilaya ya Mbeya, – Paulo Ntinika amehimiza vikundi hivyo kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.
Akikabidhi mikopo hiyo Ntinika amesema kuwa kiwango hicho cha mikopo kilichotolewa ni mfano wa kuigwa na halmashauri nyingine za mkoa huo, katika kutumia vizuri mapato ya ndani kuwawezesha wakazi wake.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Mbeya vijijini Stephen Katemba amesema kuwa mikopo iliyotolewa ni ya awamu ya kwanza na kuahidi kuviwezesha vikundi vingi zaidi vya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu ifikapo mwezi June mwaka huu.