Makamishna wa ardhi wasaidizi wa mikoa nane nchini wametakiwa kujitathimi kutokana na kushindwa kutoa taarifa ya uhakiki wa mashamba katika muda uliopangwa.
Kauli hiyo imetolewa mkoani Dar es Salaam na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula
wakati wa kikao kazi cha makamishna wa ardhi wasaidizi wa mikoa 26 nchini.
Waziri Mabula aliagiza ufanyike uhakiki wa mashamba na kupatiwa taarifa ifikapo mwezi Julai mwaka huu, ambapo Katibu Mkuu aliongeza muda huo hadi Agosti 15 mwaka huu taarifa hizo ziwe zimewasilishwa.
Makamishna wa ardhi wasaidizi wanaotakiwa kujitathmini ni wa mikoa ya Arusha, Dodoma, Geita, Kagera, Njombe, Shinyanga, Simiyu na Songwe.
Hadi Dkt. Mabula anakutana na Makamishna hao ni mikoa 17 pekee iliyowasilisha taarifa za uhakiki wa huo mashamba.