Mume amchoma visu mkewe mara 17

0
315

Mkazi wa eneo la Lukirini, kata ya Kalangalala wilayani Geita, Amina Hassan (34), amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Geita baada ya kudaiwa kuchomwa visu mara 17 maeneo mbalimbali ya mwili wake.

Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Geita, Ally Kitumbu amethibitisha kutokea kwa tukio.

Amemtaja mtu anayedaiwa kufanya kitendo hicho kuwa ni Mashaka Jeremia, ambaye ni mume wa mwanamke huyo.

Kaimu Kamanda Kitumbu amesema, mwanaume huyo alitorokea kusikojulikana mara baada ya kufanya ukatili huo.

Amesema tukio hilo limetokea Agosti 30 mwaka huu, ambapo mwanamke huyo alichomwa visu maeneo ya tumboni, ubavuni na mkononi.

Jeshi la polisi mkoani Geita linaendelea kumtafuta mwanaume huyo na mwili wa mwanamke huyo umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Geita.