Vodacom Tanzania na kasi ya 5G

0
911

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, imezindua rasmi teknolojia ya kasi ya 5G na kuifanya kuwa kampuni ya kwanza ya simu za mkononi kuitambulisha teknolojia hiyo hapa nchini.

Uzinduzi huo umefanyika mkoani Dar es Salaam, mbapo mgeni rasmi akiwa ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye.