Kilimanjaro wavuka lengo la Sensa

0
166

Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Nurdin Babu amesema mkoa wake umevuka lengo la uhesabuji wa watu katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linaoendelea nchini nzima.

Akitoa taarifa ya zoezi hilo wakati akitoa salamu za mkoa huo katika kikao kazi cha maafisa waandamizi wa Jeshi la Polisi wa makao makuu, makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi Babu amesema zaidi ya kaya laki nne zimehesabiwa Mkoani humo.

Babu amesema, kwa sasa wanaendelea na zoezi la kuhesabu majengo na muitikio wa zoezi hilo ni zaidi ya asilimia mia moja