Faida za kiafya za kuvaa kipini

0
474

Uvaaji kipini ni moja ya urembo unaopendwa sana na wanawake wa jamii mbalimbali.

Kwa miaka ya hivi karibuni kipini kimeendelea kuvaliwa sana, huku utoboaji ukifanyika katika maeneo mbalimbali ya pua ili mradi tu kipini kikae tofauti na ilivyozoeleka hapo awali.

Kwa hapa Tanzania wanawake wengi wanaovaa kipini puani ni wale wa Pwani, na wengi wanaotoboa pua hutoboa zaidi upande wa kushoto.

Baadhi ya makala zilizoandikwa kuhusu utoboaji wa upande wa kushoto wa pua zinasema yafuatayo;

• Hupunguza maumivu ya tumbo wakati wa hedhi na kusawazisha hedhi zisizo na mpangilio.

• Husaidia kuimarisha afya ya mfumo wa uzazi

• Hupunguza maumivu wakati wa kujifungua.

• Hupunguza maumivu ya kipandauso.

• Huboresha viungo vya uzazi.

Tovuti ya onmanorama inaelezea kuwa zipo neva zinazohusiana na mfumo wa uzazi ambazo huishia kwenye pua, hivyo kutoboa pua huziamsha neva hizo kufanya kazi bora zaidi.