Zoezi la sensa lafikia 95% Mtwara

0
218

Mkoa wa Mtwara umekamilisha zoezi la sensa ya watu na makazi kwa asilimia 95.

Mratibu Msaidizi wa sensa wa mkoa wa Mtwara, Patrick Kyaruzi amesema hayo baada ya kutembelea na kukagua zoezi hilo katika mitaa mbalimbali iliyopo kwenye manispaa ya Mtwara, Mikindani.

Amesema kinachoendelea kwa sasa ni kufanya uhakiki kwa kupita katika kaya ambazo zilishahesabiwa kubaini kama kuna mtu amesahaulika ili aweze kuhesabiwa na kukusanya taarifa.

Kwa upande wao baadhi ya makarani wa sensa wamesema, zoezi la sensa limekuwa rahisi kwao kutokana na mwamko wa wananchi kujitokeza kuhesabiwa.