Rais Samia atoa pongezi kwa Simba Queens

0
995

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa pongezi kwa Simba Queens kwa kunyakua ubingwa wa Afrika Mashariki wa CECAFA 2022 kwa wanawake (SAMIA CUP).

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Rais Samia amesema timu hiyo imejenga heshima ya soka la Tanzania na kuwatakia kila la kheri katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake yatakayofanyika nchini Morocco.