Ujumbe wa ADC watembelea TBC

0
186

Ujumbe wa chama Chama cha Alliance For Democratic Change (ADC) ukiongozwa na Mkurugenzi wa Fedha wa chama hicho Taifa Hassan Mvungi, umetembelea ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), zilizopo Mikocheni mkoani Dar es Salaam.

Lengo la ziara hiyo ni kujionea utendaji kazi wa shirika hilo hasa katika jukumu lake kubwa la kuwahabarisha wananchi masuala mbalimbali.

Akizungumza mara baada ya kutembelea vitengo mbalimbali na kuona namna vinavyotekeleza majukumu yake Mvungi amesema, TBC inafanya kazi nzuri na kwa weledi katika kuwahabarisha watanzania.

Wangine wamewashauri watanzania kujitokeza kuhesabiwa katika sensa ya watu na makazi inayoendelea nchini kote hivi sasa, huku serikali ikishauriwa kutoa elimu zaidi kwa wananchi kuhusu suala la tozo.

Wanachama hao wa ADC wametembelea TBC ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa chama hicho.

Chama Cha Alliance For Democratic Change
kilianzishwa mwaka 2012, ambapi tangu kuanzishwa kwake kimekuwa kikishiriki chaguzi mbalimbali nchini.