Gesi asilia kuzalishwa Ntorya

0
180

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeanza mchakato wa kuanza kuzalisha gesi asilia katika eneo la Ntorya lililopo katika kata ya Nanguruwe mkoani Mtwara.

Mkurungenzi Mtendaji wa TPDC Dkt. James Mataragio ameyasema hayo wakati wa ziara ya wajumbe wa bodi mpya ya shirika hilo, waliotembela eneo la Ntorya kujionea shughuli zinazoendelea.

Dkt Mataragio amesema uzalishaji wa gesi utaanza baada ya miezi 18 kuanzia sasa, ambapo kiasi cha futi za ujazo milioni 60 zitakuwa zinazalishwa kwa siku.

Gesi hiyo iligundulika mwaka 2012.

Kwa mujibu wa Dkt. Mataragio, kwa sasa TPDC ipo katika mazungumzo na kampuni ya uchimbaji ya ARA, ambayo itahusika katika shughuli za uzalishaji wa gesi hiyo.