14 wafariki baada ya kunywa pombe

0
755

Watu 14 wamefariki dunia nchini Uganda dunia baada ya kunywa pombe inayodhaniwa kuwa na sumu.

Polisi nchini Uganda inawashikilia watu wanne kufuatia vifo hivyo, huku kiwanda kinachotengenezapombe hiyo kikifungwa hadi hapo uchunguzi utakapokamilika.

Baadhi ya watu waliodhurika baada ya kunywa pombe hiyo inayodaiwa kuwa na sumu akiwemo muuzaji wa pombe hiyo ijulikanayo kama “City 5 – Pineapple Flavoured Gin”, wamelazwa hospitali wakiendelea kupatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi nchini Uganda, tayari sampuli za pombe zimechukuliwa kwa uchunguzi zaidi.