Mwisho Septemba Mosi mabasi yasiyotumia tiketi za mtandao

0
125

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) imesema kuanzia Septemba Mosi mwaka huu mabasi yanayofanya safari za mikoani na nchi jirani yasiyotumia tiketi za mtandao hayataruhusiwa kufanya shughuli za usafirishaji wa abiria.

LATRA imesema itatoa adhabu ya faini au kusitisha huduma ya mabasi yote yatakayoshindwa kutimiza takwa hilo ifikapo tarehe hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa LATRA Habibu Suluo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maendeleo ya mchakato wa matumizi ya tiketi mtandao kwa mabasi yanayokwenda mikoani na nchi jirani.

Amesema kipindi cha majaribio ya matumizi ya tiketi mtandao kilikuwa kuanzia Aprili Mosi hadi Juni mwaka huu, lakini LATRA kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa usafirishaji walikubaliana kuongeza muda.

Suluo amesema LATRA iliongeza muda wa miezi miwili hadi Agosti 31, muda ulioenda pamoja na utoaji wa elimu kuhusu suala hilo na kwamba changamoto zilizokuwa zikijitokeza katika mchakato huo zimeshafanyiwa kazi.

Hadi tarehe 17 mwezi huu, jumla ya mabasi 2,033 kati ya 3,916 yaliunganishwa na tiketi mtandao na kubaki mabasi
1, 883.