Watu 26 wamefariki dunia na wengine wengi wamejeruhiwa, kufuatia moto wa msituni unaoendelea kuwaka nchini Algeria.
Katika taarifa yake wizara ya Mambo ya Ndani ya Algeria imeeleza kuwa, watu 24 wamefariki dunia katika mji wa El Tarf na wengine wawili katika mji wa Setif.
Habari zaidi kutoka nchini Algeria zinaeleza kuwa, vikosi vya zimamoto na uokoaji nchini humo vinaendelea na jitihada za kuuzima moto huo.
Takribani watu 350 wamehamishwa kutoka katika makazi yao na kupelekwa maeneo salama kufuatia moto huo.
Kila mwaka Algeria imekuwa ikikumbwa na matukio ya moto wa msituni, huku sababu kubwa ikielezwa kuwa ni mabadiliko ya Tabianchi.