Kagaigai: Siasa ilikwamisha utatuzi wa migogoro ya ardhi Kilimanjaro

0
192

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai amesema changamoto kubwa mkoani humo ni uwepo wa migogoro ya ardhi ambayo mingi ilikuwa ni ya kisheria lakini baadhi ya viongozi wameigeuza na kuwa ya kisiasa jambo lililokuwa likikwamisha migogoro hiyo kumalizika.

Kagaigai ameyasema hayo mjini Moshi katika hafla ya makabidhiano ya ofisi kati yake na Mkuu wa mkoa mpya, Nurdin Babu.

Kagaigai amesema kutokana na hali hiyo iliwalazimu migogoro yote ya ardhi yenye mazingira ya kisiasa kuitatua kisheria kama inavyotakiwa kwani migogoro ya kisiasa imekuwa ni migumu kuimaliza.

“Mfano mgogoro wa Kilari kati ya wananchi na Shirika la Kazi wa Roho Mtakatifu wilayani Siha nao ulitengenezwa katika mazingira ya kisiasa jambo lililochangia mgogoro huo kudumu kwa zaidi ya miaka 40 lakini kwa kutumia sheria nimefanikiwa kuumaliza mgogoro huo,” alisema Kagaigai.

Kwa sasa Kagaigai ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).