Utafiti waendelea Mji Mkongwe

0
157

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Simai Mohammed Said akipatiwa maelezo na Profesa Mark Horton ambaye anafanya utafiti kwenye eneo la Mji Mkongwe unaoonesha kuwa watu walianza kuishi katika eneo hilo tangu karne ya 10.

Katika utafiti anaoendelea kuufanya, vimegundulika vifaa vilivyokuwa vilitumiwa na watu wa kwanza kuishi katika eneo la Unguja Ukuu katika karne hiyo ya 10.

Utafiti huo pia unaonesha kuwa, wakazi wa Unguja Ukuu walihamia katika eneo la Mji Mkongwe, na eneo linalofanyiwa utafiti kumeonekana mabaki ya miili ya watu pamoja na kuta za majengo ya msikiti na kanisa la zamani.