Madrid mabingwa UEFA Super Cup

0
174

Klabu ya soka ya Real Madrid imefanikiwa kushinda ubingwa wake wa 5 wa UEFA Super Cup baada ya kuilaza Frankfurt ya Ujeruman kwa mabao 2-0.

Matokeo hayo pia yam pa nafasi Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti akuweka rekodi ya kuwa kocha ambaye ameshinda taji la UEFA Super Cup mara ya nne na kuwa kocha pekee aliyeshinda taji hilo mara nyingi zaidi kihistoria ya michuano hiyo mbele ya Pep Guardiola aliyeshinda mara tatu.

Ancelotti ameshinda Super Cup mara mbili akiwa kocha wa AC Milan (2003 na 2007) na Real Madrid mara mbili (2014 na 2022).