Mkuu wa mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini na kumuhamisha kituo cha kazi, kuongoza Njombe.
“Mheshimiwa Rais Watanzania wapo zaidi ya milioni 60, na vijana wenye sifa nilizonazo mimi wako wengi sana. Mheshimiwa Rais una mikoa 26 Tanzania Bara, umeona ikakupendeza mimi kuwa miongoni mwa watu 26 watakaokusaidia kwenye mikoa.” amesema Mtaka na kuongeza kuwa
“Mheshimiwa Rais kwa dhati ya moyo wangu naomba nikushukuru sana naheshimu heshima hii uliyonipatia, naheshimu uteuzi huu ulionipatia. Mheshimiwa Rais ahadi yangu kwako na kwa Mungu wangu nitatumia vipaji vyangu vyote kuweza kutoa mchango wangu kwa wananchi laki nane wa mkoa wa Njombe.”