Shule sasa kufunguliwa Agosti 15

0
191

Serikali ya Kenya imesogeza mbele muda wa kufunguliwa kwa shule nchini humo, ambapo sasa zitafunguliwa tarehe 15 mwezi huu badala ya ile ya awali ambayo ni tarehe 11 ya mwezi huu.

Muda huo wa kufunguliwa kwa shule umebadilishwa ili kupisha ukamilishwaji wa mchakato wa uchaguzi mkuu uliofanyika hapo jana.

Waziri wa Elimu wa Kenya, George Magoha amesema, serikali imefikia uamuzi huo baada ya kuwapo kwa mijadala juu ya shule hizo kufunguliwa kesho wakati bado shughuli za uchaguzi zikiendelea.

Shule nyingi za msingi na sekondari nchini Kenya ndizo zinazotumika kama vituo vya kupigia na kuhesabu kura.