Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa amemuagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi kumpangia majukumu mengine Meneja wa uwanja wa Benjamin Mkapa, Godon Nsajigwa, kutokana na kushindwa kusimamia matumizi endelevu ya uwanja huo.