Afisa mwandamizi wa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Lameck Daniel amesema kwa kipindi cha manonesho ya wakulima Nanenane wamepata mrejesho mzuri wa elimu kwa umma kuhusu ulipaji wa kodi kwa wakulima
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari Jijini Mbeya katika viwanja vya John Mwakangale alipokuwa akitoa tathimini ya maonesho ya sherehe za wakulima maarufu nanenane katika upande wa ulipaji kodi za serikali.
Amesema kupitia maoni waliyopata kutoka kwa wananchi waliotembelea banda lao wamepata mirejesho mingi kutoka kwa wananchi hao ya namna ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi hao.
Ameongeza kuwa wakulima waliojitokeza kupata elimu hiyo wameweza kufahamu ni aina gani ya misamaha ya kodi iliyoachiliwa na Serikali na kodi zipi zitakazoendelea kulipwa na wakulima hao.
Aidha amewakumbusha wakulima wanaofanya biashara ya mazao na mauzo yao kwa mwaka kuzidi milioni nne watatakiwa kulipa kodi ya bidhaa zao.