Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema kufuatia vifo vya watu 16 vilivyotokea katika ajali ya gari.
Ajali hiyo imetokea katika kata ya Mwakata wilaya ya Kahama, ambapo kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Leonard Nyandahu jumla ya watu waliofariki dunia ni 16 na majeruhi 11.
Pia Rais Samia amewapa pole wafiwa wote na kusema anaungana na familia hizo katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na kwa vyombo vinavyosimamia usalama barabarani amevitaka kuongeza juhudi za kudhibiti ajali.